Severino wa Settempeda

Mt. Severino katika mavazi ya kiaskofu alivyochorwa na Vittore Crivelli, 1482 hivi.

Severino wa Settempeda (Settempeda, leo San Severino Marche, Italia 470 hivi - Settempeda, 545) alikuwa Mkristo ambaye, alipofiwa wazazi wake, aliamua pamoja na ndugu yake Viktorini wa Camerino kuwagawia maskini urithi wao mkubwa na kwenda kuishi upwekeni kwenye Mlima Nero.

Papa Vigili alimfanya yeye askofu wa Settempeda na Viktorini askofu wa Camerino (Italia ya Kati)[1].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Mei[2].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/90943
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy